Watu kadhaa wanao daiwa kuwa ni majambazi jana walivamia Benki ya NMB tawi la Mkuranga mkoani Pwani na kupora fedha kisha kumuua askari mmoja na kutokmea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafary Mohamed alithibitisha jana jioni kupata taarifa za tukio hilo.
“Taarifa hizo nimezipata kuwa watu hao wanaodhaniwa majambazi wamevamia Benki ya NMB, Mkuranga na kupora fedha ambazo kiasi chake bado hakijafahamika kisha kumuua askari mmoja aliyekuwa nje ya uzio wa eneo hilo la benki," alisema Jafary .
Hata hivyo alisema askari aliyeuawa hakuwa kazini ila walinzi wote wa benki wapo salama na silaha zao hazikuchukuliwa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment