Home
Β»
Lowassa
Β» Lowassa Azidi Kupata Mapokezi Makubwa Kila Anakoenda.......Songea Alazimika Kukaa Juu ya Paa la Nyumba, Asema Jina Lake Haliwezi Kukatwa
WAZIRI Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa amesema hana shaka na swala la kukatwa jina lake katika vikao vya Chama cha Mapinduzi(CCM), kwani anaamini Chama chao kitatenda haki kwa kurudisha jina lake kuwa mgombea urais wa Tanzania.
Lowassa aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika ofisi kuu za CCM Mkoani humo, wakati akitoa shukrani baada ya kudhaminini na wanaCCM zaidi ya elfu 52.
"Nimekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1977 nilipomaliza chuo kikuu, sijawahi kufanya kazi nje ya CCM hivyo nakijua chama na hakuna mgombea atakayeweza kuvunja rekodi ya utendaji wangu katika chama, sasa leo anayetaka kukata jina langu anatoka wapi? anakata kwa sababu gani? Sioni kosa la kukatwa jina na Watanzania hawaoni, kwa hiyo msiwe na wasiwasi jina litarudi tu". alisema Lowassa.
Lowassa aliwasili Mkoani Ruvuma mapema jana mchana akitokea Mkoani Iringa kwaajili ya kusaka wadhamini katika mbio zake za kusaka urais kwa tiketi ya chama hicho, ambapo umati wa watu ulifurika kumlaki na kupelekea kufunga barabara kuu ya mjini, hali iliyompelekea Lowassa kupanda juu ya paa la jengo la ofisi ya CCM Mkoa ili aweze kuzungumza nao.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- PICHA: Mkapa Awakutanisha Rais Magufuli na Lowassa Kwenye Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya Ndoa yake na Mama Anna Mkapa28 Aug 20160
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa leo tarehe 27 Agosti, 2016 ameadhimish...Read more ?
- Hotuba ya Edward Lowassa alipokuwa Iringa Jana25 Aug 20160
Leo(Jana) nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza kuwa tu...Read more ?
- Lowassa Apigilia Msumari Oparesheni UKUTA......Asema Haiwezekani Mtu Mmoja Azuie Kila Kitu23 Aug 20160
Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation ...Read more ?
- Lowassa atembelea shule iliyoungua moto Arusha19 Aug 20160
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA jana alitembe...Read more ?
- Lowassa Akoleza Moto CCM....Awataka Wanaomuunga Mkono Ndani ya CCM Waendelee Kumpa Siri za Serikali29 Jul 20160
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ana uhakika kuwa bado kun...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment