March 17, 2025 10:58:39 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.

Akizungumza na mtandao huu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.

“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape.

Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010.

Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema ni Ndumbagwe Misayo "Thea" (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 Jun 2015

Post a Comment

 
Top