Home
»
Stori muhimu
» Bajeti Kuu ya Serikali yapita, mafuta bei palepale.....Malipo Wastaafu Kila Mwezi sasa ni 100,000
BUNGE limepitisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2015/16 kwa asilimia 83.
Bajeti hiyo, ilipitishwa jana mchana mjini Dodoma, baada ya wabunge kuipigia kura kwa kuitwa majina mmoja baada ya mwingine.
Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, alisema wakati upigaji kura unaanza, Bunge lilikuwa na wabunge 262, lakini walipokuwa wakiendelea idadi iliongezeka kutoka idadi hiyo hadi kufikia 294.
Kutokana na idadi hiyo, alisema wabunge waliopiga kura ya ndiyo ni 219 na walioikataa ni wabunge 74.
Pamoja na idadi hiyo, alisema mbunge mmoja alitoa kauli iliyoonyesha hakushiriki kupiga kupiga kura.
“Wakati Bunge linaanza kupiga kura, ukumbini kulikuwa na wabunge 263,baadaye waliongezeka na kufikia 294.
“Wabunge 59 hawakupiga kura na waliopiga kura ya hapana ni 59,waliopiga kura ya ndiyo ni wabunge 219 ambao ni sawa na asilimia 83.
“Pamoja na takwimu hizi, mbunge mmoja alisema ni abstain kwa maana kwamba hakukubali wala kuikataa bajeti,” alisema Dk. Kashilila ingawa hakumtaja mbunge huyo.
Lakini taarifa zinaonyesha ni Mbunge wa Mpanda Mjini,Said Amour Arfi (Chadema).
Pamoja na matokeo hayo, kivutio kikubwa bungeni kilikuwa ni Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) kuikataa bajeti kuu ya Serikali kwa mara ya kwanza tangu Bunge la 10 lilipoanza mwaka 2010.
Kitendo hicho cha Mrema ambacho hakikutarajiwa, kiliamsha shangwe kutoka kwa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa kuwa waliamini angeendelea kuiunga mkono kama alivyofanya kwa miaka minne iliyopita.
Pamoja na Mrema, wabunge wengine waliosababisha kelele za shangwe bungeni kutoka kwa wabunge wa CCM baada ya kupiga kura ya ndiyo ni Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (Chadema), Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF) na Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP).
Wakati bajeti hiyo ikipitishwa, baadhi ya wabunge wa upinzani walionyesha kutoridhishwa nayo kwa kile walichosema kuwa haina jipya kwa vile haiwalengi wananchi.
Akitoa maoni yake kwa waandishi wa habari, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alisema bajeti hiyo ilipita kwa sababu kuna wabunge wengi wa CCM.
Kutokana na hali hiyo, alisema kuna haja ya wananchi kuwachague kwa wingi wagombea wa upinzani, wakati wa uchaguzi mkuu ili Bunge lijalo lisitawaliwe na chama kimoja kama ilivyo sasa.
Naye Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, kama alivyosema Mbowe, naye hakuonyesha kuridhishwa na bajeti hiyo kwa kile alichosema haitaweza kutekelezwa mwaka huu kutokana na uwepo wa uchaguzi mkuu.
Awali akitoa ufafanuzi wa hoja za wabunge walizozitoa wakati wanachangia bajeti hiyo iliyowasilishwa wiki iliyopita, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alizungumzia tozo ya Sh 100 iliyopendekezwa na Serikali katika mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa.
Kwa mujibu wa Mkuya, Serikali inatarajia kukusanya Sh bilioni 276 kutokana na tozo hiyo na kwamba fedha zitakazopatikana zitapelekwa kwenye miradi ya umeme vijijini na katika miradi ya maji.
“Lengo la Serikali ni kuwapelekea wananchi umeme katika maeneo yao na ndiyo maana tumeona ni bora wachangie shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta hayo.
“Kwa kuwa lengo letu ni hilo, wenzetu wasiifanye kama hoja ya kujiongezea umaarufu kwa sababu Sh bilioni 276, zitakapopatikana, Sh bilioni 90, zitapelekewa kwenye miradi ya maji na zitakazobaki zitapelekewa kwenye miradi ya umeme,” alisema Mkuya.
Kuhusu malipo ya pensheni kwa wastaafu, alisema Serikali imeyaongeza kutoka 50,000 walizokuwa wakilipwa kwa mwezi hadi Sh 100,000.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar22 Jan 20160
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya kuru...Read more ?
- Rais Dkt. Magufuli Amteua Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.21 Jan 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ...Read more ?
- JANUARY MAKAMBAASHANGAZWA NA HAYA MAGAZETI MATATU KUHUSU LOWASSA02 Sep 20150
Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameonesha kushangazwa na mfa...Read more ?
- Polisi Yakamata Majambazi 38 Yakiwa na silaha Nzito pamoja na Milioni 170......Majambazi hayo yanadaiwa na mafunzo ya Kijeshi01 Sep 20150
Jeshi la Polisi limewakamata watu 38 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi ambao pia wamepatiwa mafun...Read more ?
- Wananchi Wafunga Barabara Baada ya Gari la Polisi Kugonga Wanafunzi wawili31 Aug 20150
Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya...Read more ?
- Hali Tete Bunda, Viongozi CHADEMA Wajiuzulu...Kisa Ester Bulaya22 Aug 20150
SIKU chache baada ya mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maend...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment