Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
AZAM FC imekata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mabingwa Yanga SC jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo, unaifanya Azam FC ifikishe pointi 48 baada ya kucheza mechi 25, nyuma ya mabingwa, Yanga SC wenye pointi 55 za mechi 25.

Simba SC ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 44 na hata ikishinda mechi yake ya mwisho itafikisha 47, hivyo kwa mwaka wa tatu mfululizo Wekundu wa Msimbazi watakosa michuano ya Afrika.
Azam FC ilitoka nyuma kwa 1-0 baada ya Mbrazil Andrey Coutinho kutangulia kuifungia Yanga SC dakika ya 12 na Bryson Raphael akasawazisha dakika ya 14 kabla ya Aggrey Morris kufunga la ushindi dakika ya 85.

Kikosi cha azam kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Gadiel Michael, Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Mudathir Yahya, Brison Raphael, Frank Domayo, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche na Brian Majwega.  

  YangaFC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Saum Telela, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Amissi Tambwe, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho
Mchezo uliisha na mabigwa Yanga kukabidhiwa kombe tazama picha hapa chini:














76532 1 4

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
06 May 2015

Post a Comment

 
Top