Inawezekana Irene Uwoya ameamua kuweka sehemu ya historia ya maisha yake kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram na kuamua kushare na Watanzania.
Kwa mujibu wa sehemu ya maelezo yake ni kama anataka kuwaelezea watu kuhusu sehemu ya maisha yake aliyoyapitia kipindi cha nyuma licha ya kuishia katikati na kusema kuwa ataendelea tena.
Hii ni sehemu ya kwanza ambayo Irene ameiweka kwenye ukurasa wake.
INAENDELEA...bunge na kumaliza la saba!nikaenda kidato cha kwanza st.thomas gongolamboto mpaka kidato cha pili badae nikaenda Uganda nikasoma mpaka kidato cha 3 nikarud bongo kuchukua pass mpya coz yakwanza ilikuwa imesha isha…..ilikuwa ijumaaa nikiwa nimeenda kwajili ya pass mpya nirud shule!!!ndipo nilikutana na kaka mmoja mrefu,mweusi akaniita malaika”nikashangaa mhh mbona sio jina langu ?akanisogelea a kanambia kwa lugha ya kingereza Naitwa Patrick ponce monzanga!nikawa na nashangaaa coz sikuwa namjua’nikamwambia naitwa irene akanambia naomba nikwite malaika coz ur sooo beautiful huku akinipa mkono…nilipo mpa mkono tuuu basiii kumbe nilikuwa nimejitengenezea bomu bila kujua…..ITAENDELEAAAaaaaaaaaa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment