March 19, 2025 08:44:56 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Reporter wa wetu alikuwa mmoja ya watu wa kwanza kupewa taarifa juu ya tukio hili, akafika Kunduchi ambako Ali Kiba na mdogo wake Abdu Kiba wanaishi.
Nimeongea na Abdu Kiba, amesema yeye alikuwa Masaki, Ali akampigia simu kwamba kuna watu kama 15 hivi wamevamia nyumbani kwao.. waliovamia waliruka ukuta saa tisa usiku, wakavunja mlango wa sebuleni, wakakuta vijana wawili ambao wanaishi nao, wakawapiga na kuwalazimisha wawaoneshe chumba ambacho Ali yumo.. wale vijana wakajibu kwamba Ali hayupo, wakaulizia chumba chake wakaoneshwa chumba cha Abdu Kiba.
Wameingia chumbani wakamkosa Ali Kiba, wameiba vitu vingi vya sebuleni na chumbani pia, pamoja na pesa milioni 2 na nusu zilizokuwa chumbani kwa Abdu.
Askari walifika na kukagua, wakaondoka na kuahidi kwamba wanafanya upelelezi.






Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
02 May 2015

Post a Comment

 
Top