June 20, 2025 03:14:27 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
PAMOJA na tetesi kuwa nguli wa filamu za Kibongo Blandina Chagula ‘Johari’, ameshindwa kushika mimba, mwenyewe ameamua kufunguka na kudai kuwa kizazi chake kinafanya kazi na anachosubiri ni kumpata mwanaume ambaye atakuwa tayari kumuoa ndipo atakaporuhusu kuzalishwa.

 
Nguli wa filamu za Kibongo Blandina Chagula ‘Johari’.

Akizungumza na Amani, Johari alisema kuwa endapo akitokea tayari yupo ndani ya ndoa anaweza kufanya hivyo lakini kwa maneno ya watu kamwe watasubiri kwani anaamini kizazi chake kipo imara na wakati wowote akiamua kushika mimba kitafanya kazi.

“Kizazi changu kinafanya kazi na mipango hiyo ya kushika mimba mimi siwezi kukubali nipate mtoto kabla ya kuolewa, suala la kufanya jambo kwa lengo la kuwafurahisha watu mimi siwezi kufanya hivyo,” alisema Johari.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
18 Dec 2014

Post a Comment

 
Top