March 15, 2025 08:13:26 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Wakazi mbalimbali wa Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto, Mkoani Tanga wamesema kuwa wapo tayari kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba kama ataamua kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa Uraisi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Wakazi hao ambao walionyesha nia yao hiyo katika sehemu mbalimbali alizopita Mbunge huyo katika ziara yake ya siku sita kutembelea jimbo lake iliyoanza Machi 30. Makamba ni mmojawapo wa watu wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ya Urais.

Alipokuwa katika kata ya Tamota, viongozi wa dini walimfanyia maombi maalum ambayo yaliongozwa na  Mchungaji Amasia Mweta na Sheikh Amiri Yahaya Shekibula mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutumbiwa na Mbunge huyo kijana.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Bumbuli katika  maeneo yote  aliyopita  kwenye ziara yake, Makamba aliwashukuru wakazi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kusema kama sio wao asingeweza kuonekana na kutajwa katika kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa CCM.

Makamba, huku akishangiliwa na wakazi hao wa maeneo  hayo, alisema kuwa hakuna namna ambayo unaweza kutengeneza watu kukutaja katika nafasi za juu bila kupitia kwa wananchi kukuchagua katika nafasi ya kuwawakilisha.

“Kutajwa si dhambi na kwa kuwa fomu za uchaguzi sio sumu si dhambi  pia kuchukua na kuingia katika kinyang’anyiro hicho,” alisema na kuongeza kuwa sasa hivi kuna kiu kubwa ya uongozi wa aina mpya na kuna watu wamemuona na kumtaja yeye jambo ambalo si baya. 

Nao wananchi , wakiwemo vijana, kina mama na wazee katika maeneo mbalimbali aliyopitia Makamba, walimhakikishia Mbunge huyo kuwa hivi sasa hawatampokea mtu yeyote ambaye atakuja kujipitisha katika jimbo hilo hadi hapo watakapojua hatma ya utekelezaji wa nia ya Mbunge huyo kuwania nafasi ya kuwa mgombea wa Urais kupitia  CCM.

Nao waumini wa Usharika wa Bumbuli walimtaja Mbunge huyo kuwa jasiri, mweledi na mwenye maono mapana na wakasema wanaahidi kuwa bega kwa bega katika harakati hiyo  ya kuwania kuwa mgombea wa CCM.

 
Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na wazee mara baada ya kuwasili jimboni kwake.


Mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri Sayansi na Teknolojia, January Makamba akipokelewa na akina mama na kupewa baraka zake.  

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
06 May 2015

Post a Comment

 
Top