
West Brom imewachabanga mabingwa ligi kuu ya England Chelsea jumla ya mabao 3-0 hali ambayo kwa sasa inaifanya klabu hiyo kukaa eneo salama zaidi dhidi ya kushuka daraja.
Katika mechi hiyo iliyochezwa, dimba la The Hawthons, Saido Berahino alikata utepe wa magoli kwa kufunga goli la kwanza mnamo dakika ya 9,na pia dakika ya 47 Berahino tena akaweka kimiani goli la pili kwa njia ya penati ,baada ya kuangushwa na John Terry eneo la adhabu na hivyo hadi mwisho wa mchezo West Brom 3 Chelsea mabingwa nunge. Kwa matokeo hayo West Brom sasa wamefanikiwa kukaa eneo salama kuepuka kushuka daraja,huku Chelsea wakiwa bado mabingwa. Kesho Arsenal watakwaana na Sunderland.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment