Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, amekabidhiwa hundi ya zaidi ya milioni 14 kwa ajili ya kufidia ujenzi wa upande wa nyumba yake uliodondoka.
 
Wakati akikabidhiwa mfano wa hundi hiyo na Kampuni ya Bima ya UAP kwa ushirikiano na Benki ya CRDB, Diamond alisema ukuta wa nyumba yake ulianguka wakati akiwa anamuuguza mama yake aliyekuwa katika hali mbaya.
 
“Ilikuwa ghafla ukuta wa nyumba yangu ya Tegeta ukaanguka wakati huo nilikuwa natakiwa kulipia fedha kwa ajili ya kurekodi wimbo wangu mpya.
 
“Hivyo nisingekuwa nimejiunga na bima sijui sasa ningekuwa kwenye hali gani? Ni kipindi kigumu sana kwangu,’’ alieleza Diamond huku akiwataka Watanzania wajiwekee bima kwa kuwa ina msaada mkubwa unapopatwa na majanga mbalimbali ya vitu ulivyokatia bima hiyo.
 
Naye, Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa UAP, Raymond Komanga, aliwasisitizia Watanzania waondoe fikra za kwamba bima inayokatwa ni ya gari pekee bali wakate bima za aina mbalimbali.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top