Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Uhusiano kati ya Davido na Diamond Platnumz ulishavunjika siku nyingi kufuatia issue iliyotokea mwaka jana kwenye fainali za shindano la Big Brother Africa.



Davido na Diamond Platnumz akiwa studio mwishoni mwa mwaka juzi

Tukio hilo lilimfanya Davido aandike mfululizo wa tweets za mafumbo ambazo wengi waliamini kuwa ni madongo kwa Diamond aliyewahi kumshirikisha kwenye remix ya Number One iliyotokea kuwa hit namba moja Afrika miaka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kambi ya Diamond ilisisitiza kuwa hakuna ugomvi kati ya mastaa hao wawili na hata staa huyo wa ‘Nasema Nawe’ hivi karibuni aliwahi kuupa shavu wimbo mpya Davido kwenye Instagram.

Lakini vipi kama kweli Davido na Diamond bado ni washkaji? Kwa kile alichokipost Davido kwenye ukurasa wake wa Facebook, huenda wawili hao wakawa wanaendelea kupanga kufanya makubwa baadaye.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Davido amepost picha ya zamani akiwa na Diamond kwenye studio yake nchini Nigeria. Kwenye picha hiyo, Davido ameandika: I think I just recorded a sweeter love song than AYE .. Hmm this album yo.”
~Bongo5

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top