Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 Wanachama Saba (7) wa klabu ya Simba ya Dar es salaam kutoka tawi la Mpira na Maendeleo (maarufu kama Simba UKAWA) ambalo limewahi kutangazwa kufutwa wamefariki dunia katika ajali ya basi mkoani Morogoro.

Mashabiki saba (7) wa timu ya soka ya simba ya jijini dar es salaam wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya costa kwenda mkoani shinyanga kushuhudia mechi baina ya timu hiyo na wakata miwa wa Kagera Sugar, kuacha njia na kupinduka katika eneo la kwa Makunganya, barabara kuu ya Morogoro - Dodoma.

Mashuhuda wa ajali hiyo waliokutwa eneo la tukio, wameiambia wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni  utelezi uliosababishwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha, uliomfanya dereva wa gari waliyokuwa wamepanda aina ya costa, yenye namba za usajili T304 CWN kushindwa kumudu na kuserereka kwa karibu kilometa 15, kabla ya kuvaa ukingo wa barabara na kupinduka na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo Rehema Musa na Mohamed Kigolini maarufu kama ngumi jiwe, huku wengine wakijeruhiwa 
Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zimebainisha kuwa majeruhi watatu kati ya 15 wa ajali hiyo hali zao zilikuwa ni mbaya, na wote wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu,huku dereva wa gari hiyo akitokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03.
Asakari wa kikosi cha usalama barabarani akichukua taarifa.
Wanachama wa simba wakiwa katika majonzi makubwa 


Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top