March 15, 2025 01:21:00 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, amenusurika  kuuawa  jana  mchana  na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.

Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi.

Mashuhuda wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.

Baada ya kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
24 Apr 2015

Post a Comment

 
Top