March 15, 2025 08:13:26 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
article-3053583-27EF38BC00000578-394_964x390Hatimaye wanafunzi wa zamani wa kocha wa Manchester United – Louis Van Gaal, katika klabu ya FC Barcelona watapata nafasi ya kuonyeshana umwamba katika kuelekea jijini Berlin Ujerumani ambapo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya itachezwa.
Ratiba ya nusu fainali ya michuano hiyo imepangwa muda mfupi uliopita, huko Nyon – Uswiss.
Ratiba inaonyesha Luis Enrique ataiongoza FC Barcelona kukipiga dhidi ya FC Bayern Munich inayofundishwa na mchezaji mwenzie wa zamani wa Barca – Pep Guardiola.
Guardiola na Luis Enrique walikuwa kwenye kikosi kimoja cha Barca kilichokuwa kikifundishwa na Van Gaal msimu wa 1999/2000.
Kwa upande mwingine mabingwa watetezi wa kombe hilo, Real Madrid watacheza dhidi ya Juventus. Mechi za raundi ya kwanza zitachezwa Mei 5 na 6 na marudiano zitakuwa wiki moja itakayofuatia ya tarehe 12 na 13.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
24 Apr 2015

Post a Comment

 
Top