Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kiongozi  wa  chama  cha  ACT-Tanzania,Zitto Kabwe  amesema  kuitwa  msaliti  ni  mbinu  zinazotumika 'kumuua' mwanasiasa  wa  upinzani  nchini.

Amesema  mwanasiasa  wa  upinzani  akitakiwa  kuuawa  kisiasa  si  jambo  geni  kusikia  anatuhumiwa  kutumika  na  Usalama  wa  Taifa  au  Pandikizi  la  Chama  cha  Mapinduzi, CCM.

Akizungumza  na  wahariri  wa  vyombo  vya  habari   jijini  Dae  es  Salaam  juzi,Zitto  alisema  kauli  kama  hiyo  ilitumika  kumshusha  kisiasa  mjumbe  wa  kamati  kuu  ya  CHADEMA, Mabere Marando  na  Mwenyekiti  wa  NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

"Si  jambo  jipya, mmesahau  kwamba  Mbatia  aliitwa  pandikizi,leo  Mbatia  yuko  wapi,si  yuko  meza  moja  na  UKAWA?

"Mmesahau  baada  ya  serikali  ya  Umoja  wa  kitaifa  juzi  tu  hapa  kwamba CUF  waliitwa  CCM-B, mmesahau  kwamba  CUF  waliitwa  mashoga, leo  kiko  wapi?

"Mmesahau  Marando  aliitwa  pandikizi, tena  dhidi  ya  Mrema(Mwenyekiti  wa  TLP),leo  Marando  ni  shujaa  na  Mrema  tunamtukana.Hizi ni  siasa  tu  na  zitaendelea  tu," alisema

Aidha  alisema  kuna  watu  wengine  wataibuka  baadaye  nao  wataanza  kulaumiwa, kama  Mwalimu Nyerere  alivyosema.....Ukishakula  Nyama  ya Mtu  Huachi.

Kutokana  na  hali  hiyo  alisema, walioitwa  wasaliti  wametoka  huko  walikokuwa  na  watasikika  wasaliti  wengine  wanaibuka  kwa  sababu  siasa  iko  hivyo..

"Juzi  nimemsikia  Halima Mdee  anasema  mimi  siyo ACT,ninyi  mliwahi  kuandika  kama  Halima  ni  ACT,hiyo  maana  yake  nini,inamaanisha  kuna  presha  anapigwa  huko.

"Angalau  Shibuda  ni  mtu  ambaye  haeleweki  misimamo  yake  ni  nini, lakini  hivi  ni  vitu  vya  kawaida,"alisema.

Akizungumzia  kutumiwa  na  vyombo  vya  usalama,Zitto  alisema  yeye  kama  kiongozi  hawezi  kuacha  kuwasiliana  na  watu  wa  usalama  wa  Taifa.

"Huwezi  kuwa  kiongozi  wa  chama  kikubwa  kinachojiandaa  kushika  dola  usiwe  na  uhusiano  na  Mkuu  wa  Jeshi  la  Polisi,Mkuu  wa  jeshi  la  wananchi  au Mkuu  wa  Usalama  wa  Taifa,utakuwa  ni  kiongozi  wa  ajabu  sana." Alisema

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top