Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Tukio la mauaji ya limetokea Mbeya, inahusu tukio la mwanaume mmoja kumuingila kinguvu msichana wa miaka 8.
Mwanaume huyo alimuita msichana na kumuagiza dukani akamnunulie mafuta, aliporudi alimuingilia kinguvu, akamuua halafu akautupa mwili wake kwenye shimo.
Mama wa mtoto huyo amesema alirudi mwenye mizunguko yake lakini hakumkuta mtoto huyo, akaanza kumtafuta.. alipowauliza wenzake walisema alikuwepo nyumbani baada ya kurudi shuke lakini hawajui baada ya hapo alielekea wapi.
Akaamua kutoa taariifa Polisi na kwa Balozi wa nyumba kumi, wakaitisha kikao.. baadae vijana wakaanza kumtafuta na kukuta mwili wake ukiwa kwenye shimo.
Baada ya siku tatu wanakijiji walianza msako na kukuta baadhi ya vitu vya marehemu nyumbani kwa mwanaume mmoja zikiwemo nguo pamoja na damu, kwa hasira wakaanza kumshambulia kwa kipigo na kuchoma moto nyumba hiyo hadi Polisi walipofika na kuwazuia.
Polisi walimchukua mtuhumiwa huyo na kumpeleka kituoni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top