Zuwena
Abdul (29), Mkazi wa Buzebazeba, Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambaye jana
alijifungua mapacha wanne katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni.
Bi.
Zuwena Abdul, mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Buzebazeba, Manispaa ya Kigoma
Ujiji, anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema, serikali na asasi mbali mbali
za kijamii, ili aweze kuwatunza watoto wake mapacha wanne aliojifungua.
Zuwena
anaomba msaada huo kutokana na kwamba hana kipato chochote kumudu kuwatunza
watoto wake kwani yeye ni mama wa nyumbani na mume wake Rajabu Mkangwa,
anajishughulisha na shughuli ndogo ndogo za uzalishaji.
Ingawa
amesema anajisikia faraja kujifungua mapacha hao, lakini changamoto iliyoko
mbele yake ni namna ya kuwalea kutokana na familia yake kuishi maisha duni.
Mama
mzazi wa Zuwena, Jaqlina Augustino, mkazi wa Gungu Manispaa ya Kigoma Ujiji,
amesema uzazi wa mwanae wa kujifunga mapacha wanne uliwashitua mno, kwani licha
ya familia za pande zote mbili, yaani upande wa Zuwena na ule wa mume wake kuwa
na historia ya mapacha lakini haijawahi kutokea mtu kuzaa mapacha wanne.
“Kwa
kweli hicho kitu kilitushangaza sana na pamoja na hayo tunashukuru Mungu sana
kuona ni maajabu kuzaa kawaida wakati wengine mtoto mmoja tu wanafanyiwa
operation, lakini yeye Mungu akatenda miujiza akazaa kwa njia ya
kawaida,”alisema mzazi wa Zuwena.
Afisa
Muuguzi Msaidizi katika Hospitali ya Maweni, Agnesi Nguvumali, alisema Zuwena
alijifungua kwa njia ya kawaida mapacha wanne jana majira ya saa kumi na mbili
jioni, ambao kati yao watatu ni wa kiume na mmoja wa kike,ambapo amesema kuwa
mtoto wa kwanza amezaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.8, wa pili kilo 2.5, wa tatu
1.7na wa nne kilo 1.7.
“Tunawatunza
kwa njia ambayo tunaita Kangaroo, kama ambavyo Kangaroo yule mnyama anavyotunza
mtoto wake kifuani,”alisema Agnesi.
Alisema
aina hiyo ya utunzaji kwa ngozi ya mama na mtoto kugusana, inamsaidia mtoto
kupata uzito mkubwa kwa sababu ya joto la mama tofauti na njia zilizokuwa
zikitumiwa hapo mwanzo ikiwemo ya kuvundika.
“Kikubwa
tunachoomba yule mama kama alivyosema ni mama wa nyumbani, angeweza kusaidiwa
hasa kwenye maziwa ili aweze kutunza hawa watoto wakaweza kukua; kwa yeyote
atakaeguswa aweze kumsaidia huyu mama,”aliongeza afisa muuguzi huyo.
Kaimu
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, Fadhili
Kibaya, alisema mpaka sasa hali za watoto hao pamoja na mama yao zinaendelea
vizuri.
Kufuatia
kujifungua mapacha hao wanne, Bi. Zuwena sasa amefikisha idadi ya watoto 8
kwani kabla ya mapacha hao yeye na mume wake tayari walikuwa na watoto wengine
4.
Kwa
yeyote mwenye kuguswa na ana nia ya kumsaidia Zuwena Abdul, tafadhali wasiliana
nae kwa namba za simu zifuatazo: 0759 558472.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar22 Jan 20160
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya kuru...Read more ?
- Rais Dkt. Magufuli Amteua Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.21 Jan 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ...Read more ?
- JANUARY MAKAMBAASHANGAZWA NA HAYA MAGAZETI MATATU KUHUSU LOWASSA02 Sep 20150
Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameonesha kushangazwa na mfa...Read more ?
- Polisi Yakamata Majambazi 38 Yakiwa na silaha Nzito pamoja na Milioni 170......Majambazi hayo yanadaiwa na mafunzo ya Kijeshi01 Sep 20150
Jeshi la Polisi limewakamata watu 38 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi ambao pia wamepatiwa mafun...Read more ?
- Wananchi Wafunga Barabara Baada ya Gari la Polisi Kugonga Wanafunzi wawili31 Aug 20150
Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya...Read more ?
- Hali Tete Bunda, Viongozi CHADEMA Wajiuzulu...Kisa Ester Bulaya22 Aug 20150
SIKU chache baada ya mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maend...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment