Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Staa wa filamu Bongo, Lungi Maulanga hivi karibuni ametoa ushuhuda wake kwamba alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kujisaidia kitandani mpaka alipofika kidato cha pili lakini alipona katika mazingira ya kushangaza.
 
Akizu-ngumza  na mwandishi wetu Lungi alifunguka: “Nikiri tu kwamba nilikuwa kikojozi mpaka nafikia form two, nilikuwa naona aibu sana lakini aliyenisaida ni bibi mmoja ambaye aliniponya katika mazingira ya kushangaza.
 
“Baada ya kumwambia tatizo langu, aliniambia nipande kwenye mti wa muembe nikiwa na nguo zangu, nikiwa juu akaniambia nikojoe kisha nishuke.
 
“Niliposhuka, akaniambia nibadili nguo na kusema tatizo langu limeisha, sikuamini lakini ukweli ni kwamba kuanzia siku hiyo sikujisaidia tena kitandani.”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top