SIYO siri! Huku jana akiwa ametarajiwa kuripoti tena Kituo Kikuu cha Polisi, Dar (Central) kauli ya serikali kwamba, taasisi za dini ambazo viongozi wake wamekuwa wakitoa matamshi yenye mlengo wa kisiasa zitafutwa mara moja kwani ni kinyume na sheria ya usajili inadaiwa kumpa presha Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Juzi, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya waumini wa makanisa mbalimbali ya kiroho ya jijini Dar ambao walieleza kuwa, kauli hiyo inamgusa Mchungaji Gwajima kwa vile ndiye ambaye hivi karibuni alitoa maneno yenye mweleko wa kisiasa.
“Mimi nadhani Gwajima ndiye mwenye presha. Maana yote yaliyosemwa ndiyo ambayo yeye amehusika nayo, kuhusu maneno ya kisiasa na mrejesho wa uendeshaji wa kanisa lake, mambo ambayo ametakiwa kuwasilisha baadhi ya nyaraka pale Alhamisi ijayo (jana) kwenye Kituo cha Polisi cha Central,” alisema Yohana Petro, mkazi wa Mwenge.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, mchungaji mmoja wa kanisa la Gwajima alidai:
“Watu wanaweza kufikiria kwamba Mchungaji Gwajima ana presha lakini sidhani kama hali iko hivyo. Suala la viongozi wa dini kutoa matamko ya kisiasa ni la kidunia. Viongozi wa dini wanatakiwa kukemea maovu ya nchi.
“Gwajima yuko imara, yupo ngangari na Neno la Mungu. Yeye ni mwakilishi wa kazi za Mungu kwa wanadamu!” alisema mchungaji huyo.Jumanne iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, alisema kuwa, sheria ya usajili wa taasisi za dini zinakataza viongozi wake kujihusisha na mambo ya kiimani.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Audio: Gwajima afyatuka tena, amshauri Magufuli aihame CCM....Adai amenasa njama Mbaya14 Jun 20160
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye anafahamika kwa kutoa kauli ‘tat...Read more ?
- Gwajima: Dk. Slaa Basi Tena Ametekwa na Mke Wake Josephine Mushumbusi na Haiwezekani Kumtoa09 Sep 20150
Gwajima ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema Dk. Willibrod Slaa ...Read more ?
- Kauli ya Askofu Gwajima Yamtokea Puani....Aulizwa Malimao Aliyosema Sasa yako Wapi ? Ni Kuhusu Kauli Aliyotoa Arusha Kwenye Mkutano wa LOWASSA23 Jul 20150
Katika Mkutano wa Lowassa Huku Arusha wa Kutangaza nia ya Urais Mchungaji Askofu Gwajima wa Kani...Read more ?
- Gwajima: Asiyempenda Lowassa Akale Limao!!!01 Jun 20150
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephati Gwajima amesema kwamba mwananchi au...Read more ?
- Gwajima, Flora Mbasha waibukia mkutano wa CHADEMA Kawe, ni ule wa kuzindua kitabu cha Mbunge25 May 20150
MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, na mwibaji nguli wa muziki wa Injili Fl...Read more ?
- Upelelezi Kesi ya Askofu Josephat Gwajima Mbioni Kukamilika05 May 20150
UPELELEZI wa kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Mchungaji Josephat Gw...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment