March 17, 2025 10:32:12 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Jenerali Muhammadu Buhari anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan 

Matokeo ya awali ya kura zilizopigwa siku ya jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari
anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan.
Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos.

 Kwa kuongeza, mgombea wa APC (Buhari) amepata walau asilimia 25 ya kura zilizopigwa kwenye theluthi mbili ya majimbo 36 ya Nigeria. Buhari pia ameshapata zaidi ya kura 14,855,820 dhidi ya 12,107,628 za Jonathan.

Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao.
Huku zaidi ya nusu ya matokeo yakiwa yametangazwa mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari yuko mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
31 Mar 2015

Post a Comment

 
Top