March 28, 2025 05:52:43 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baada ya kutemwa na CHADEMA, Zitto Kabwe aenda jimboni kwake Kigoma Kaskazini kuzungumza na wananchi wake. 


LOL na haya ndio mapokezi aliyopata huko jimboni, watu nyomi wamejitokeza kumpokea na kelele zikisikika ..ZITOO...ZITOOO..ZITOOO...


MANENO MENGINE MAGUMU AMBAYO ZITTO AMEWAAMBIA WANA KIGOMA LEO AKIWA KWENYE ZIARA YAKE......

Ikiwa bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa  vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali.

        Akiwa katika ziara yake  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa makini  walishapitia misuko suko kama yake.


       Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya Chama chake na yeye
Zitto ametoa kauli hiyo leo mjini Kigoma alipokutana na viongozi 250 kwenye mkutano wa ndani uliohusisha viongozi  kutoka katika kila kijiji kwenye jimbo la Kigoma kaskazini yenye jumla ya vijiji 45.

Aliwataja baadhi ya  wanasiasa waliopita katika hatua kama yake na baadae wakageuka washindi kuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad(Tanzania),Mahathir Mohamed(Malaysia na Indira Gandhi wa India.

              “Msinililie mimi kwa kuwa haya ni mapito ya kila mwanasiasa Makini,wengi walio makini walitofautiana na vyama vyao kwa sababu ya maslahi ya mataifa yao,wapo walioanzisha vyama baada ya hali hiyo na wakashinda na wapo waliopigiwa magoti na vyama vyao baada ya kugundua walichofanya si sahihi, hivyo jukumu kubwa ni kuniunga Mkono”alisema Zitto.

            Alisema mpaka sasa hajapewa taarifa yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake na kama hali hiyo ikijitokeza atarudi kuwafahamisha juu ya hatua atakayochukua.

             Zitto yupo mjini Kigoma kwa ziara ya siku tatu,ambapo atawatembelea wakulima wa mradi wa Kahawa walio katika mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF), pamoja na kukabidhi gari aina ya Ambulance katika kituo cha Afya Nyarubanda na kisha kufanya mikutano miwili ya hadhara.
       
          Juzi Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu,alitangaza hadharani kuvuliwa uanachama kwa Zitto kutokana na kushindwa katika kesi aliyofungua kupinga asijadiliwe na Chama Chake

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 Mar 2015

Post a Comment

 
Top