Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Picha aliyoweka Faiza Ally Instagram ya Mhe. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ akiwa katika pozi na mwanaye Sasha.
MSANII wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo amewatolea uvuvi watu waliokuwa wakijiuliza maswali kuhusu mwanaye Sasha na na baba yake.
Baada ya kuweka picha ya Sugu na mwanaye, Faiza Ally aliandika haya.
Kupita akaunti yake ya Instagram, Faiza ameweka picha na Mhe. Sugu akiwa na mwanaye Sasha na kuandika kuwa     "Mara nyingi huwa nawapiga picha mimi mwenyewe sema tu sipendi sana kurusha kwangu"
Na kwa wale waliokuwa wanauliza maswali juu yao, Faiza amewajibu hivi: "Ni kweli kuna wakati tulikuwa hatuelewani kabisa na wala hatukuwa tunaonana lakini kwa sasa tofauti zetu zimeisha hatuna ugomvi japo hatuko pamoja"
Faiza akiwa na Mhe. Sugu enzi hizo.
"Lakini mwisho wa siku huyo ndiyo baba Sasha na mzazi siku zote atakuwa mzazi tu, haijalishi tuna tofauti kiasi gani" Alimalizia kuandika msanii huyo asiyeishiwa vituko.
Baada ya kuwek picha hiyo wengi wa mashabiki wa Faiza walimpongeza kwa hatua hiyo huku wengine wakiwataka warudiane ili walee mtoto pamoja.
Baadhi ya comments za mashabiki wa Faiza Ally.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
16 Mar 2015

Post a Comment

 
Top