Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Tattoo mpya ya Nick Cannon.
Kushoto ni tattoo ya jina la Mariah Carey ikiwa mgongoni mwa Nick na kulia ni tattoo aliyochora baada ya kuachana naye.
RAPPA, komedian na mwigizaji wa Marekani, Nicholas Scott "Nick" Cannon ameamua kumfutilia mbali mkewe wa zamani Mariah Carey kwa tattoo nyingine zaidi mgongoni mwake.
Awali Nick Cannon (34) aliamua kufuta tattoo ya jina la mkewe Mariah Carey aliyeachana naye mwaka jana kwa tattoo ya mchoro wa Yesu akiwa msalabani.
Nick Cannon akiwa na mkewe Mariah Carey enzi za penzi lao.
Kuona kuwa hiyo haitosha, staa huyo ameamua kuongeza tattoo zaidi ili kumwondoa kabisa mkewe huyo akilini ambapo ameongeza michoro mingine mgongoni ikiambatana na maneno haya kwa chini "Baba, wasamehe watu hawa maana hawajui walifanyalo" maneno ambayo yatakuwa yanahusiana na ndoa yake na Mariah.
Nick na Mariah wakiwa na watoto wao mapacha Monroe na Moroccan.
Cannon na Mariah walifunga ndoa mwaka 2008 na kudumu kwa miaka sita kabla ya kuachana mwaka jana.
Katika mahusiano yao walifanikiwa kupata watoto wawili mapacha Monroe na Moroccan.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top