
Hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya UEFA Champions’ League imeanza jana kwa michezo yote kutoka sarekatika viwanja viwili tofauti.
Katika dimba la Parc des Princes nchini Ufaransa Chelsea imetoshana nguvu na PSG kwa kutoka sare ya bao 1-1.
Chelsea walikuwa wa Kwanza kupata bao kupitia kwa Branislav Ivanovic dakika ya 36 lakini kipindi cha Pili kupitia kwa Edinson Cavan PSG walisawazisha ikiwa ni dakika ya 54.

Mechi ya marudiano itapigwa Machi 11 katika dimba la Stamford Bridge, ambapo Chelsea italazimika kupata ushindi wa aina yoyote, au suluhu ya bila kufungana.

Katika mchezo mwingine Bayern Munich ya Ujerumani imeshindwa kutamba nyumbani kwa Shakhtar Donetsk Arena Lviv nchini Urusi kwa kulazimishwa suluhu ya bila kufungana.

Katika mchezo huu Bayern wamelazimika kucheza pungufu kuanzia dakika ya 65 baada ya kiungo wao Xabi Alonso kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Mchezo wa marudiano utafanyika Fußball Arena München Machi 11, 2015 ambapo Bayern italazimika kushinda ili kuingia Robo Fainali.
Michezo ya Leo ni
Basel Vs FC Porto
Schalke 04 Vs Real Madrid
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment