Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

DullyMarehemu Mzee Abby Sykes ambaye ni Baba mzazi wa mwimbaji wa Bongo Fleva Prince Dullysykes, alifariki saa 8 mchana February 15 2015 akiwa hospitali ya taifa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Dullysykes ameongea na millardayo.com ikiwa ni pamoja na kuelezea kitu kilichosababisha umauti wa baba yake ambapo ameanza kwa kusema >>’Mzee alikua ana vidonda katika miguu na ndiyo chanzo kikubwa, sumu ikasambaa ikasababisha kifo chake, vidonda vilishindwa kupona kwa ajili ya moshi wa sigara ila zaidi hakuwa na tatizo jingine lolote manake baba yangu alikua strong’
abby sykes
Alianza kuugua vidonda miezi minne iliyopita, miezi miwili alikua anavumilia tu lakini miezi miwili ya mwishoni ndiyo vilizidi kumsumbua, mazishi tunategemea kuyafanya February 16 2015 leo saa kumi jioni kwenye makaburi ya Kisutu lakini safari ya kwenda msikitini tutaanza saa 7 mchana‘ – Dully.
Mzee Sykes alizaliwa mwaka 1952. #RIP #MzeeWetu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top