Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

SENEGAL-VOTE
Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo ameamua kujiondoka kutoka chama tawala cha PDP, kinachotarajia kushiriki kwenye uchaguzi march 28, na kuamua kuichana kadi yake ya uanachama hadharani.

Rais huyo wa zamani amekuwa mmoja ya wafuasi wa chama tawala cha PDP ambao wamekuwa wakimkosoa Rais Goodluck Jonathan, ambaye anawania awamu ya pili ya Urais wa nchi hiyo.
Obasanjo aliichana kadi yake ya uanachama huku akiwaambia kwamba waichukue yeye haihitaji tena kadi hiyo, hii haikupokelewa vizuri na inasemekana kuna mpasuko ndani ya chama katika kipindi hiki cha mwisho wakati uchaguzi ukiwa unakaribia.
images
Obasanjo amesema kuwa hatojiunga na chama chochote atabaki kuwa  raia wa kawaida na yuko tayari kuchangia maendeleo ya taifa kwa kushirikiana na mtu yeyote bila kujali msimamo wa kisiasa.

Rais Goodluck Jonathan amemlaumu Obasanjo kwa kukipigia debe chama kikuu cha upinzani All Progressives Congress (APC).

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top