March 27, 2025 10:26:24 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Lady Jaydee ameendelea kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa kupitia EATV.
“SWALI: Una watoto wangapi?

JIBU : Sina mtoto wala watoto

SWALI:Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa

SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao.

SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ?
Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeye
Anaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania

SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.
Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini
Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11
Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia.

SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?
JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio
Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
18 Feb 2015

Post a Comment

 
Top