
Kundi la Dola ya Kiislamu katika Iraq na Sham (ISIS) limemuua kwa kumchoma moto rubani wa Jordan, Moaz al-Kassasbeh.
Kundi hilo lilitoa masharti kwa serikali ya Jordan kuwaachia huru wanachama wake wawili Sajida al-Rishawi na Ziyad Karboli.
Katika mkanda wa video wa dakika 22 uliorushwa na kundi hilo umemuonesha Moaz mwenye umri wa miaka 26 akiwa amevaa mavazi ya rangi ya machungwa huku akiwa amezungukwa na moto.
Moaz alikamatwa na kundi hilo Desemba 24, 2014 baada ya ndege yake aina ya F-16 ilipoanguka wakati ikiruka kaskazini mwa Syria katika harakati za kijeshi dhidi ya kundi hilo.
Serikali ya Jordan imelipa kisasi kwa kuwanyonga Sajida al-Rishawi na Ziyad Karboli.






Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment