Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baada ya hapo juzi Waziri Lazaro Nyalandu kupitia Clouds FM kukanusha tuhuma  zilizokuwa zimezagaa kwenye magazeti  na mitandaoni za kuwa anachepuka na mwigizaji wa filamu hapa bongo, Aunty Ezekiel na kusisitiza kuwa yeye sio  muhusika wa ujauzito wa mwigizaji huyo, nikaamua kupitapita  kwenye kurasa za  mcheza shoo wa Diamond, Moses Iyobo ambae ndio anasemekana kuwa  yeye ndio amempa ujauziko mwigizaji  huyo.
Kwanza nilikutana na andiko la malalamiko kutoka kwa Iyobo, ambae alikuwa ameweka picha ya Aunty na kuandika haya;
“Kama kumpenda nampenda sana lakini kinacho nipasua kichwa mie kuni save dalali kwenye cm yake yani sielewi ata kidogo”
Lakini kilichonipa faraja ni picha hiyo hapo juu akiwa na Aunty kitandani na kuandika ule msemo kutoka Yamoto Band ambao unamaanisha mtu akipenda amependaaa.
‘Nzi kufa kwenye kidonda sio ufala ila..........’
Kwa picha na ujumbe huu ni wazi Iyobo ndio baba kijacho kutoka kwa Aunty Ezekiel.
Mzee wa Ubuyu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
15 Feb 2015

Post a Comment

 
Top