March 16, 2025 07:54:18 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya kidia one lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea jijini Mwanza kugongana uso kwa uso na lori la mizigo lililokuwa likitoka Dodoma kwuelekea Morogoro katika kijiji cha vikonje kata ya mtumba nje kidogo ya mji wa Dodoma.

ITV ilifika eneo la ajali ambapo mashuhuda wa ajali hiyo akiwemo dereva msaidizi wa basi aliyejitambulisha kwa jina moja la Makubeli akisema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi kuharibika mfumo wa breki na kumshinda dereva mwenzake kauli inayopingana na mmoja kati ya abiria aliyekuwemo kwenye basi hilo ambaye anadai chanzo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita basi jingine lililokuwa mbele yao bila tahadhari na ghafla akakutana uso kwa uso na lori.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Sasp David Misime amesema chanzo cha ajali kimetokana na dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T 663 AXL aina ya Scania alipokuwa akijaribu kulipita gari lingine bila kuchukua tahadhari na kukutana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T 496 CFG likiwa na tela namba T 576 AXZ ambapo watu wawili waliofahamika kwa majina ya Fadhili Saidi dereva wa lori na Chogo Chigunda utingo wa basi wakafariki dunia.
 

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Dodoma Dk Nasoro Mzee amethibitisha kupokea maiti hizo mbili na majeruhi 44 ambapo 16 wametibiwa na kuruhusiwa huku wengine 27 wakilazwa.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
19 Feb 2015

Post a Comment

 
Top