March 18, 2025 06:43:21 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Baba mzazi wa Dully Sykes, Mzee Ebby Sykes amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62. Angetimiza miaka 63 February 24.
10958102_336497629887424_191661160_n
Mtoto wake wa kike aitwaye Raya Sykes amethibitisha taarifa hizo kwenye mtandao wa Instagram.
“Mungu akulaze mahali pema peponi baba angu mm nilikupenda lakin mungu alikupenda zaid nasikitika nipo mbali sitaweza kukuzika!ulikua ni mtu mwenye upendo na kila mtu alikupenda nakupenda sana baba angu R I P dady nitakukumbuka milele daima,” ameandika Raya.
Bado hakuna taarifa rasmi za sababu za kifo cha Mzee Sykes. Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae Dully.
“Uncle Ebby Sykes i love u…. in life and in death…'” ameandika mpwa wake, Basillah Sykes.
Mzee Sykes alizaliwa tarehe 24 February, 1952.
‎Mungu ailaze roho yake mahali pema.
Abby Sykes akiwa na mtoto wake Dully Sykes
Abby Sykes akiwa na mtoto wake, Dully Sykes

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
15 Feb 2015

Post a Comment

 
Top