
Baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya wamekua wakitumianyumba za vigogo wakubwa wanazopanga kama kichaka cha kuficha dawa hizo. Imefahamika.
Uchunguzi umebaini baadhi ya dawa za kulevya wamekua wakipanga nyumba za viongozi ili kukwepa polisi wasiwapekue nyumbani pindi wanaposhukiwa.
Imeelezwa kwamba imekuwa desturi kwa polisi, wakijua kuwa nyumba fulani inamilikiwa na kiongozi fulani wa nchi wanaacha kuipekua kwa kumuheshimu na kudhani kuwa mpangaji ana undugu na kiongozi huyo na wakati mwingine kuogopa tu.
Mkuu wa kitengo cha Polisi cha kuzuia dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alikiri kuwepo kwa suala hilo na kusema kuwa kikosi chake kilifanikiwa baada ya kukiuka utaratibu huo wa kuheshimu nyumba za viongozi na kukamata shehena ya unga ikiwa imehifadhiwa katika baadhi ya nyumba.
MWANANCHI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment