March 24, 2025 11:44:42 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mchezaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo akiwa na tuzo ya Ballon d'Or baada ya kutangazwa na FIFA kuwa Mwanasoka Bora wa mwaka 2014.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter (kulia) akimpongeza Ronaldo baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo.
Mchezaji bora wa Dunia, Ronaldo (kushoto) akiwa na mchezaji bora wa kike, Nadine Kessler.
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kutangazwa mshindi.
Cristiano Ronaldo (kushoto) akisalimiana na Rais wa UEFA, Michel Platini.
Ronaldo (kushoto) na Messi (katikati) wakiwa wamekaa pamoja.
Mchezaji wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo.
Ronaldo ameshinda kwa kupata 37.66% ya kura zote zilizopigwa, akifuatiwa na Lionel Messi aliyepata 15.76% wakati @Manuel_Neuer akipata 15.72% ya kura zote.
MCHEZAJI wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo ametangazwa mshindi wa tuzo ya FIFA ya Mwanasoka Bora wa mwaka 2014 maarufu kama FIFA BALLON D'OR ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.
Ronaldo amewashinda Lionel Messi wa Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina pamoja na golikipa wa timu ya taifa ya Ujerumani na Bayern Munich manuel Neuer.
Ronaldo ameshinda kwa kupata 37.66% ya kura zote zilizopigwa, akifuatiwa na Lionel Messi aliyepata 15.76% wakati @Manuel_Neuer akipata 15.72% ya kura zote.
Katika Tuzo hizo, kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low ametajwa kuwa Kocha bora wa FIFA wa mwaka 2014, na James Rodrigues amepata tuzo ya bao bora la FIFA la mwaka 2014 na kutunukiwa tuzo ya FIFA PUSKAS AWARD kwa bao aliloifungia Colombia katika mchezo wa Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay.
Kikosi bora cha FIFA ni Neuer: Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
13 Jan 2015

Post a Comment

 
Top