Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa Muungano wa Afrika AU akichukua nafasi ya Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania.
  
Mugabe mwenye umri wa miaka 90 ameteuliwa kwa kauli moja na Wajumbe katika mkutano wa AU unaoendelea kwa sasa mjini Addis Ababa-Ethiopia.
 
Imeelezwa kuwa uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arobaini, huenda ukaleta doa ndani ya AU, kwa kuwa Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa madarakani tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mwaka 1980.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top