June 20, 2025 06:59:07 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
FBL-ITA-SERIEA-JUVENUS-SCUDETTO-CEREMONY

Kocha wa klabu ya Juventus Masimiliano Allegri amechochea tetesi za kuondoka kwa nyota wake Paul Pogba baada ya kuwataka mashabiki wa klabu hiyo kumtazama Pogba kwa kipindi hiki wakati akiwa Juventus kwani huenda wasipate nafasi hiyo tena .
Pogba mwishoni mwa wiki iliyopita alifunga bao moja huku akisaidia kutengeneza bao jingine katika mechi ya Juventus dhidi ya Chievo Veron amechi ambayo Juve walishinda 2-0 ukiwa muendelezo wa kiwango bora ambacho ameendelea kukionyesha tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Manchester United .
Tetesi mbalimbali zimemhusisha Pogba na kujiunga na klabu kadhaa barani ulaya zikiwemo Paris St Germain , Real Madrid , Manchester City , Chelsea na Manchester United ambazo kwa nyakati tofauti zimehusishwa na nyota huyo .
Pogba mwenyewe ameonekana kuziongeza kasi tetesi hizi baada ya kusema kuwa angependa kurudi Manchester United huku kwa wakati mwingine akisema kuwa ameanza kujifu nza lugha ya kihispania ambapo kauli hiyo imehusishwa na mpango wa kujiunga na mabingwa wa ulaya .
Paul Pogba amekuwa akizungusha vichwa vya makocha mbalimbali wa timu kubwa barani ulaya kwa kiwango alichoonyesha akiwa na Juventus .
Paul Pogba amekuwa akizungusha vichwa vya makocha mbalimbali wa timu kubwa barani ulaya kwa kiwango alichoonyesha akiwa na Juventus .
Nyota wa zamani wa Juventus na Real Madrid Zinedine Zidane amehusishwa kwenye mapgno wa kumshawishi Pogba kujiunga na Real Madrid ambapo hivi karibuni gwiji huyo alisikika akisema kuwa mar azote Madrid inasajili wachezaji nyota .
Juventus tayari wanaonekana kujiandaa kumpoteza nyota huyu baada ya kocha wa timu hiyo kusema kuwa hakuna kinachomzuia mchezaji hasa kama anapatikana kwa bei itakyoleta faida kwa klabu .
Juventus wameweka bei ya paundi jmilioni 77 kwa ajili ya nyota huyu toka kwa timu yoyote itakayotaka kumsajili ambapo Juventus itatumia fedha hizi kusajili nyota wengine watatu au wanne ili kujiimarisha zaidi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
27 Jan 2015

Post a Comment

 
Top