Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mshauri wa masuala ya ulinzi katika Benki Kuu (BoT), Shaban Ndosi (39) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kujaribu kumuua ofisa wa Polisi.

Ndosi alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema. 
 
Wakili wa Serikali, Janeth Kitali alidai kuwa Oktoba 21, 2014 katika eneo daraja la Salender karibu na mataa ya kuongoza magari, alijaribu kumuua askari Polisi, Koplo Salehe.
 
Hakimu Lema alisema mshitakiwa hatakiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na upelelezi umeshakamilika hivyo kesi itahamishiwa Mahakama  Kuu.
 
Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika waliosaini hati ya dhamana ya Sh milioni mbili pia alitakiwa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria. Kesi hiyo itatajwa tena Februari 23 mwaka huu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top