Mmiliki wa Blog moja Saudi Arabia amehukumiwa kifungo na kuchapwa viboko hadharani kwa kukutwa na hatia ya kuandika habari katika tovuti yake iliyodaiwa kuitukana Dini ya Kiislamu pamoja na kushinikiza wananchi wa nchi hiyo kukataa utawala wa kidini.
Raif Badawi ambaye ni mwanzilishi wa Blog hiyo inayoitwa Liberal Saudi Networkamehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na kuchapwa viboko 1000 hadharani, ambapo kila wiki atakuwa akichapwa viboko 50.
Watu katika mitandao ya kijamii na waharakati wameandika ujumbe wa kuchukizwa kuhusiana na hukumu aliyopewa Blogger huyo kwa kuandika ujumbe wenye hashtags “#FreeRaif, #IStandWithRaif na #JeSuisRaif.“
Mbali na hukumu hiyo, Badawi aliamriwa pia kulipia faini ya dola 226,000 huku mwanasheria wake akihukumiwa miaka 15 jela kwa makosa mbalimbali.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment