Kuna taarifa zilizoenea jioni ya leo January 10 kupitia mitandao mbalimbali, watu wametumiana picha na taarifa kwamba Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepata ajali.
Picha zilizoenea zinaonyesha Mbunge huyo amesimama na watu kadhaa pembeni ya gari aina ya Land Cruiser iliyopinduka.
Taarifa ya uhakika niliyoipata kuhusu tukio hilo ni kwamba Mbunge huyo amepata ajali akiwa na wenzake wanne ndani ya gari wakitoka Mbeya kuelekea Dar, ajali hiyo imetokea eneo la Kitonga, Iringa eneo ambalo lina kona kali za barabara.
Taarifa iliyoandikwa na mwandishi Francis Godwin kwenye matukiodaima.co.tz imesema hakuna mtu aliyefariki wala kupata majeraha makubwa ila Mbunge huyo ana michubuko midogo midogo, Kamanda wa Polisi Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment