Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Air Canada Dreamliner
Kwenye Hekaheka ya leo Jan 19 inatokea Dar inamhusu Binti mmoja aliyepelekwa Oman na mtu aliyemfahamu kwa ajili ya kufanya kazi za ndani, lakini hakuwa na maisha mazuri kutokana na manyanyaso makubwa aliyoyapata kwa bosi wake ambaye ni mtanzania anayeishi huko.
Baada ya kufanya kazi kwa wiki mbili yalianza manyanyaso kutoka kwa bosi wake na familia yake ikiwemo vitisho vya kuuwawa, alipoomba arejeshwe nyumbani walimkatalia, akaamua kutoroka.
Njiani alikutana na mtu aliyemsaidia kwenda kituo cha Polisi na baada ya maelezo bosi wake alipigiwa simu na kufika kituoni kutoa maelezo, wakafikia muafaka wa binti huyo kurudi kwa bosi wake kuendelea na kazi.
Aliporudi manyanyaso yalizidi ikiwemo bosi huyo kuwaamuru watoto wake kumdhalilisha na kumnyima mshahara, alijifanya kachanganyikiwa kwa kuanza  kupiga kelele, bosi wake akaamua kumkatia tiketi ili arudi nyumbani bila kumpa hela yoyote.
Bonyeza play kusikiliza Hekaheka yote ya leo January 19.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

Anonymous said... January 20, 2015 at 12:37 AM

Kweli wabongo wanyama, yaani huyo dada anaelezea mateso aliyopata na watangazaji walikuwa na upeo mdogo wanachambua hiyo issue bila ya kufikiria. Inaonekana hajawahi kuishi nje ya Bongo.

 
Top