Mwigizaji mrembo wa filamu hapa Bongo,Faiza Ally ameyasema hayo iliwa ni maoni yake juu ya swala la wapenzi kuitana baby.
“Leo kuna wakati nilikua nasikiliza Clouds fm nika sikia kuna wanaume hawapendi kuitwa baby!! wanahisi ni fake na wanaibiwa, kusema kweli mimi binafsi sipendi kumuita mwanaume mzima na akili zake na ndevu zake eti baby siwezi kutamka kwa sababu naona fake na mm mwenyewe sipendi kuitwa baby , kuna majina Mengi Kama honey ,darling mpenzi ni sawa japo mimi siyatumii pia binafsi napenda kumuita mtu jina lake na mimi niitwe langu au afadhali hata niitwe honey Lakini ilo pia huyo mtu awe ana maanisha sio tu mmekutana siku mbili tatu mnabandikana majina agh au uta sikia hubby , mume wangu hapo hamjaoana mpo mpo tu mahusiano hayaeleweki basi mmeshaanza kuitana mke wangu,mume wangu kweli jamani ? sio kudanganyana huko? Majina hayo kila moja Lina nafasi yake tuache ku fake sana jamani! mwisho wa siku una danganya nafsi yako na kujipa madaraka si yako!!! TAFAKARI CHUKUA HATUA”-Faiza alimaliza.
Nawe pia unamaoni gani juu ya hili?..
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment