
Muonekano wa
lori lenye namba za usajili T122 ALW baada ya kugongana na basi la
Fanuel Express yenye namba za usajili T919 DCD katika kijiji cha
Ibetelo eneo la Nyororo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Basi la Fanuel Express yenye namba za usajili T919 DCD baada ya ajali hiyo.
Zaidi ya watu 4 wamefariki na
wengine kujeruhiwa baada ya basi la abiria kutoka Mbeya kwenda Dodoma
kugongana na Lori katika kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo wilayani
Mufindi mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa
Ramadhani Mungi amesema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 4.45
asubuhi na kuhusisha basi mali ya kampuni ya Fanuel Express yenye namba
za usajili T919 ACD kugongana uso kwa uso na lori lenye namba za
usajili T122 ALW mali ya kampuni ya Transisco lililokuwa likitokea Dar
es salaam kwenda nchi jirani.
Amesema watu wawili waliokuwa
ndani ya basi wamefariki papo hapo na wote waliokuwa ndani ya lori
wanahofiwa kufa, ambapo hadi kufikia majira ya saa 7 mchana, watu wawili
ndani ya lori walikuwa wamethibitika kufariki kufanya waliokufa kuwa
wanne hadi kufikia saa 7 mchana,
Zoezi la kuondoa miili iliyokuwa ndani ya lori linaendelea ambapo amesema kuwa huenda idadi hiyo ya waliokufa ikaongezeka.
Zoezi la kuondoa miili iliyokuwa ndani ya lori linaendelea ambapo amesema kuwa huenda idadi hiyo ya waliokufa ikaongezeka.
Akielezea mazingira ya ajali
hiyo, Kamanda Mungi amesema kuwa basi hilo lilikuwa likijaribu kulipita
basi lililokuwa mbele yake katika eneo ambapo palikuwa na lori lingine
lililoharibika, wakati huo huo lori lililohusika katika ajali hiyo
lilikuwa likikwepa lori lililoharibika pamoja na basi hilo, ndipo magari
hayo yalipogongana uso kwa uso katika jitihada za kukwepana.
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mafinga
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mafinga
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment