Viongozi wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe wamemtuhumu Waziri William Lukuvi kuwa alitaka kuiba ripoti ya kamati yao kuhusu uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow.
Sakata
hilo lilihitimishwa Jumamosi wakati Bunge lilipoazimia kuwajibishwa kwa
watu wote waliohusika kwenye uchotwaji wa fedha hizo, ikiwa ni pamoja
na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa taasisi za fedha zilizoruhusu
kufanyika kwa miamala mikubwa kinyume na taratibu za kibenki.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wabunge hao wawili kutoka Chadema na CCM walilieleza Mwannchi kuwa jaribio hilo lilishindikana baada ya wao na mjumbe mwalikwa, Luhanga Mpina (CCM) kuamua kukesha wakiilinda ripoti hiyo tangu ilipokuwa ikichapwa hadi ilipowasilishwa bungeni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wabunge hao wawili kutoka Chadema na CCM walilieleza Mwannchi kuwa jaribio hilo lilishindikana baada ya wao na mjumbe mwalikwa, Luhanga Mpina (CCM) kuamua kukesha wakiilinda ripoti hiyo tangu ilipokuwa ikichapwa hadi ilipowasilishwa bungeni.
Hata
hivyo, Lukuvi alikanusha vikali tuhuma hizo akisema kuwa aliipata
ripoti hiyo siku iliposomwa na kwamba kama angehusika, asingekubaliwa
kuwa mjumbe wa kamati ya maridhiano iliyoundwa mwishoni mwa kikao
kupendekeza maazimio ya Bunge.
“Si kweli,” alisema waziri huyo wa nchi anayehusika na sera, utaratibu na Bunge.
“Unajua
PAC walikuwa wanafanya kazi chini ya hazina. Hata Spika wa Bunge
hakuiona hiyo ripoti, aliisikia tu ikisomwa bungeni. Kwanza kamati
ilikuwa ikidurufu hiyo taarifa yake eneo la mbali na ili uipate ilikuwa
ni lazima umrubuni Zitto.”
Aliongeza
kusema: “Kama kweli nilikuwa nataka kuiba taarifa yao nisingekubali
kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya maridhiano, iliyokutana kupitia upya
mapendekezo ya PAC baada ya yale ya awali kuzua mvutano bungeni.”
Hata
hivyo, Filikunjombe, ambaye alikuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo,
alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa walilazimika kumwondoa eneo la
kuchapishia ripoti hiyo.
“Waziri Lukuvi alitumwa saa 9:00 usiku kuiba taarifa yetu wakati tunaichapa. Taarifa ilikuwa katika ‘flash’ na tulipogundua hilo tulimfukuza. Sisi tuliamua kuilinda ripoti ili isiibwe,” alisema Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM.
“Waziri Lukuvi alitumwa saa 9:00 usiku kuiba taarifa yetu wakati tunaichapa. Taarifa ilikuwa katika ‘flash’ na tulipogundua hilo tulimfukuza. Sisi tuliamua kuilinda ripoti ili isiibwe,” alisema Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM.
“Ile
taarifa tuliichapa usiku wa kuamkia Jumatano ambayo ilikuwa siku ya
kuiwasilisha bungeni. Na hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya kikao cha Bunge
kuahirishwa mara tu baada ya PAC kuwasilisha taarifa yake, ili Serikali
ikajipange,” aliongeza.
Mbali
na kauli yake ya jana, Filikunjombe aligusia suala hilo la ulinzi
wakati akishukuru wabunge kwa kushikamana katika kufikia maazimio manane
ya kuwawajibisha wote waliohusika.
Katika
shukrani hizo, Filikunjombe alisema walilazimika kukesha usiku wa
kuamkia Jumamosi iliyopita kuilinda ripoti yao isiibiwe na hivyo
kuwashukuru watendaji wa Bunge kwa kazi nzuri.
Hata
hivyo, kabla ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kulienea taarifa kuna watu
waliiiba na kunyofoa kurasa zilizokuwa na nyaraka za vielelezo na
baadaye kuanza kuzisambaza. Polisi ilidai baadaye kuwa ilimkamata mtu
aliyekuwa akisambaza vitabu hivyo vya ripoti, lakini hadi leo
hajafikishwa mahakamani wala hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na polisi
kuhusu maendeleo ya mtuhumiwa huyo.
Katika
sakata hilo kubwa la aina yake, Bunge lilimtia hatiani Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mwanasheria Mkuu Jaji
Fredrick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Eliachim Maswi na
wakurugenzi wa Shirika la Umeme kwa kuhusika kwa makusudi au kwa uzembe
katika kufanikisha miamala haramu kutoka kwenye akaunti hiyo.
Bunge
pia lilitaka hatua za kisheria zishughulikie watu wote waliohusika
kwenye sakata hilo, wakiwemo wanasiasa waliopokea fedha za mgao, taasisi
za kifedha zilizohusika kufanikisha miamala haramu na wafanyabiashara
waliohusika.
Vikwazo
Akizungumzia
vikwazo walivyokumbana navyo wakati wa kutekeleza majukumu yake,
Filikunjombe alisema kamati hiyo, iliyokuwa na wajumbe 24, watatu wakiwa
waalikwa, kati yao 19 kutoka CCM na watano kutoka upinzani, walipata
vikwazo vingi ikiwa ni pamoja na jaribio la kurubuniwa.
Filikunjombe
alisema wajumbe wa PAC waliamua kuwa kitu kimoja na kuweka itikadi zao
pembeni licha ya watu mbalimbali kutumia fedha kutaka kuwagawa ili
wasisimamie ukweli. “Unajua sakata la Escrow linawagusa watu wenye fedha
ambao walianza kuuaminisha umma kuwa wajumbe wa PAC na sisi tumekula
fedha hizo. CCM ilitakiwa kuuchukulia wizi huu kama ajenda yake kuu,”
alisema.
Alisema
hakupendezwa na ushauri uliotolewa na Mbunge wa Bariadi Magharibi
(CCM), Andrew Chenge kuhusu adhabu wanazotakiwa kupewa watuhumiwa wa
wizi wa fedha hizo, wakati na yeye akiwa miongoni mwa watuhumiwa
kutokana na kudaiwa kupewa Sh1.6 bilioni.
Kuhusu
suala la watuhumiwa kujiuzulu, Filikunjombe alisema siku zote Serikali
haipendi kusimamiwa na Bunge, bali inapenda kushauriwa na kwamba hiyo
ndiyo sababu ya Serikali kukataa pendekezo la PAC la wahusika kujiuzulu
bila kuziomba mamlaka za uteuzi kutekeleza hilo.
“Ukitizama
suala la (mkataba wa ufuaji umeme) Richmond si kama fedha zilichotwa
wazi, lakini hili la escrow fedha zimechotwa na waliochota wanajulikana,
sasa iweje tushikwe na kigugumizi kutaka wajiuzulu. Tena fedha hizo ni
mara tatu ya zile za Richmond,” alisema.
Zitto ataja vitisho
Kwa
upande wake Zitto alisema: “Vitisho vilikuwa vingi, lakini siyo kutoka
serikalini bali kutoka kwa watu binafsi ambao wanahusika na uchotwaji
huu wa fedha.
“Mfano
kupigiwa simu kuambiwa niachane na jambo hili ama sivyo nitakufa au
hata kutishiwa kuchafuliwa. Vipeperushi vya matusi dhidi yangu
vilisambazwa kwenye nyumba za wabunge ili kuniondolea heshima na uhalali
wa kuongoza vikao.”
Akieleza
sababu za kuilinda ripoti, Zitto alisema: “Kwa sababu Serikali ilikuwa
inataka kuipata mapema ili kuichakachua, hatukulala siku hiyo mpaka
taarifa yetu ilipokuwa taarifa rasmi ya Bunge. Mimi, Deo na Luhaga ndio
tuliopewa jukumu hilo.”
Alisema hawakupata usumbufu kutoka serikalini, isipokuwa pale zilipoanza kujengwa hoja kuwa mahakama imezuia mjadala.
Alipoulizwa
kama watuhumiwa wa sakata hilo waliwahi kumfuata kwa namna yoyote ile
alisema: “(Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen) Masele peke yake
ndiye alikuwa akiomba msaada. Maswi alinipigia simu siku moja tu kuomba
msaada, lakini sikumjibu kitu. PAC tunaamini kuwa tumetenda haki kwa
wananchi.”
Maswi
alipopigiwa simu jana alipokea na mwandishi alipojitambulisha, alikata
simu na alipopigiwa tena kwa simu tofauti alipokea na alipoulizwa swali
hilo aliikata tena simu.
Ripoti ya PAC ilisomwa na kujadiliwa bungeni na kusababisha mtikisiko mkubwa kutokana na mapendekezo yake kuwagusa watu wazito ndani ya Serikali.
Ripoti ya PAC ilisomwa na kujadiliwa bungeni na kusababisha mtikisiko mkubwa kutokana na mapendekezo yake kuwagusa watu wazito ndani ya Serikali.
Watu
wengine waliotajwa kwenye ripoti hiyo ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na kuwavua nyadhifa zao wenyeviti
watatu wa kamati za kudumu za Bunge., Victor Mwambalaswa (Nishati na
Madini), William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala) na Andrew Chenge
(Kamati ya Bajeti).
Mapendekezo
hayo yanataka Mwambalaswa, Ngeleja na Chenge wavuliwe nyadhifa zao,
sambamba na wote waliohusika katika muamala wa Akaunti ya Escrow
kuchukuliwa hatua baada ya uchunguzi.
Credit: Mwananchi
Credit: Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment