Babalevo amewachokoza nyuki na sasa anauguza maumivu. Rapper huyo
amejikuta akipokea matusi ya kila aina kutoka kwa mashabiki wa Alikiba
waliochukizwa na ujumbe wale wa dhihaka kwa mfalme wao, hitmaker wa
‘Mwana’.

Pengine akitafuta njia ya kuongeza ucheshi kwenye ujumbe wake wa
pongezi kwa Diamond kufuatia ushindi wake kwenye tuzo za Channel O,
Jumamosi hii, Babalevo alipost picha ya kitanzi na kuandika:
Ally kiba naomba uingie mwenyewe coz umeyataka mwenyewe.. sungura
ulikuwa umesha mkamata eti umemuachia kiboya boya sasa kumkamata tena
itaghalimu miaka mitano… Sisi wote Tupo kwenye Sanaa ila nguvu
tunazidiana ndomana ally nilikuona mkombozi Wetu coz we ni fundi
muziki.. Inakuwa je unajianguaha kwenye kumi na nane?????? Badala ya
kufunga unategemea penati… Ona sasa refa kapeta… Na kufanya Kwa sasa
tukubali bwana @diamondplatnum ni #KIBOKO japo alikwapua Ka aidia kangu
na ndo kanakompa mijituzo.. Ila nime hands up… Ally kiba na diamond wote
ni ma home boy kutoka KIGOMA ila mnyonge mnyongeni Haki yake mpeni… Hii
ni kick kuna mtu yeyote mwenye snea?”
Ujumbe huo ulisababisha hasira isiyo kifani kutoka kwa mashabiki wa
Alikiba ambao kama wangeweza kumuona live muda huo, huenda angechezea
kichapo kikali.
“Hv ww unahc unaweza mfkia Aly kiba cku moja kichwa kikubwa akil
tope nngekuona wa mana ungechochea kuelewana kwao bt ndo kwanza unaongea
pumba kutafta tension au ndo kujpendekeza kwa dai kwa style hyo hv
unaelewa unachoimbaga au unafoka tu na ushkuru kigoma oll star ilkutoa
wngne tulkua ht hatukujui tulza mshono uctafte kick kwa nguvu,” aliandika mmoja.
“Hahaaaaa anaangaika huyooo maana hata mwanangu nikimuuliza
hakujui. Pyeeeeeeeeeee.unaacha kusifia tunzo iliopatikana
nikwawantanzania unaanza kutaja majina yawatu.hata Wewe siunaimba kwann
jamani kwann umseme mwenzio.jitahidi nawewe boya Wewe,” aliandika mwingine.
Mwigine aliandika: Sura yenyewe imekomaa kama ngozi ya goti mm
sijawahi kukuelewa hata cku moja kwenye kazi zako yaani nilishakusahau
kama na ww unaimba kama vp rudi kigoma ukavue dagaa kama mziki
umekushinda waache watoto kina kiba wenye mji wao mtu mkubea akili huna
jipangee.”
Baada ya kuona risasi aliyoipiga imemrudia mwenyewe, Babalevo
alijaribu kuweka mambo sawa kwa kupost picha nyingine akiwa na Alikiba
na kuandika:
“Ally kiba eeeeeeeeeeeeeeeeee niokoe babaaaaaaaa…… mashabiki wako
watanimalizaaaaaaaaaa…. Mi nilikuwa kwenye maswala ya kutoa maoni tu
babaaa……coz @diamondplatnumz ametunyooooooshaaaaaa…..sasa we ndo
#mkombozi tuliye kuchagua tuokoe babaaaaaaa…… Kachukua tuzo tatu si
unajua anatumia nguvu za GIZAAAA?
Hapana chezea mashabiki wa ‘Mwana Dar es Salaam’
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment