Wanandoa kutoka Marekani wamefunguliwa mashtaka baada ya kuwateka watoto wao wanne ambao ni wadogo kwa nguvu kutoka kwa bibi yao na kuwapeleka katika nchi nyingine ya Mexico.
Wazazi hao wameshtakiwa katika mahakama ya nchini humo kwenda jela kwa kosa hilo na mara baada ya kumaliza hukumu hiyo hawataruhusiwa kuwaona watoto hao.
Akitangaza hukumu hiyo Mwendesha mashtaka alisema mwanaume huyo kwa jina la Alex amehukumiwa jela miaka 11 huku mkewe Rose Chairez akihukumiwa miaka mitano na hawakutakiwa kujitetea.
Watoto hao ambao wawili kati yao wana miaka nane na sita na wengine wawili wa kike ni mapacha mwaka mmoja walikua wakilelewa na bibi yao baada ya wazazi wao kuwatelekeza.
Watoto hao walipatikana na kurejeshwa Los Angeles na kwa sasa watakua chini ya kituo cha kulelea watoto .
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment