Shabiki mmoja amefariki dunia huko nchini Hispania kufuatia vurugu
zilizotokea muda mfupi kabla ya mchezo kati ya Atletico Madrid na
Deportivo La Coruna .
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alifariki dunia baada ya kupata
shinikizo la damu wakati akiwa miongoni mwa wtau waliokuwa katikati ya
vurugu zilizotokea kati ya mashabiki wa timu zote mbili.
Awali uongozi wa ligi ya Hispania ulijaribu kuahirisha mchezo huo
lakini jaribio la kufanya hivyo lilizuiliwa na Shirikisho la soka la
Hispania .

Picha
ikiwaonyesha mashabiki wa Deportivo na Atletico madrid wakifanyiana
vurugu saa chache kabla ya mchezo baina ya timu hizo mbili .
Vurugu kati ya mashabiki zilitokea saa tatu kabla ya mchezo kuanza
ambapo mashabiki kadhaa waliumia wakiwemo watu 10 ambao walipata
majeraha yaliyohitaji kuwahishwa hospitalini .
Viongozi wa juu wa klabu zote 20 za ligi kuu ya Hispania wametoa
tamko la kukemea vurugu zilizotokea baina ya mashabiki wa Deportive na
Atletico Madrid nab ado haiajfahamika kama kuna hatua zozote
zitakazochukuliwa kwa timu hizo kufuatia vurugu zilizotokea .
Mchezo huo uliendelea kama kawaida ambapo Atletico Madrid walishinda
2-0 baada ya mabao yaliyofungwa na Saul Nigez na Arda Turan .
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment