Mashabiki wa Arsenal wamezungumza na kama sauti yao itasikika basi
huenda siku za Arsene Wenger kama kocha wa klabu hiyo ya London
zinahesibika .
Hii ni baada ya mashabiki wa timu hiyo kuonyesha kuwa wamechoshwa na hali ya timu hiyo kuwa nyuma ya timu nyingine .
Mabango yaliyoonekana kwenye uwanja wa Hawthorns hapo jana wakati
Arsenal ikiwa inacheza na West Bromwich Albion yalionyesha ujumbe
ulioandikwa hivi ‘Arsene Wenger We Thank You For The Memories , But Its
Time To Say Goodbye, ‘Yaani Asante kwa kumbukumbu nzuri lakini muda wa
kuagana na wewe sasa umewadia’.
Kauli hii ya mashabiki wa Arsenal inakuja baada ya timu hiyo kujikuta
ikiwa nyuma ya vinara wa ligi kuu ya England Chelsea huku kukiwa na
pointi 13 na nafasi tano ambazo zimezitofautisha timu hizi mbili .
Zaidi ya hapo mashabiki hao wakiingalia timu yao hawaoni kama wana
matumaini ya kweli ya kutwaa ubingwa wa ulaya au kufika mbali kama vile
nusu fainali , au fainali .
Tangu Arsenal walipotwaa taji la ligi kwa mara ya mwisho imepita
miaka kumi na pamoja na kutwaa ubingwa wa kombe la Fa msimu uliopita
bado mashabiki hawaoni kama chini ya Mfaransa huyu kuna matumaini ya
kweli ya kufikia kilele cha mafanikio kama ilivyo kwa timu za Manchester
City , Chelsea na Manchester United .
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro












Post a Comment
Post a Comment