Moja kati ya story zilizoshtua wapenda michezo nchini England
mwishoni mwa wiki hii ni ajali ambayo aliipata nyota wa zamani wa
Manchester United na Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England
David Beckham .
Becks alipata mkasa huo wakati akiwa anatoka kumchukua mwanae
anayefahamika kwa jina la Brooklyn toka kwenye mazoezi ya kila siku ya
timu yake ya Arsenal .

Gari la David Beckham aina ya Audi likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali aliyoipata mwishoni mwa wiki iliyopita .
Gari ya Beckham aina ya Audi iligongana na gari nyingine ndogo na
star huyo alipata jeraha kwenye bega lake japo halikuwa jeraha kubwa
sana .

Picha inayoonyesha magari mawili likiwemo la David Beckham lililopo upande wa kulia baada ya ajali aliyoipata star huyo.
Mtoto wa star huyo Brooklyn amabye ni mchezaji wa timu ya Vijana ya
Arsenal hakuumia kwenye ajali hiyo ambayo magari yote yaliyohusika
yaliharibika vibaya .
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro









Post a Comment
Post a Comment