Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Nguli wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ akiwa na Kajala Masanja.

NGULI wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ amefunguka kuwa, mastaa wengi wa kike wamemgeuza babu yao kwa kumfanyia vituko kila wanapokutana naye. 

Akitema mbili tatu na paparazi wetu baada ya kusambazwa kwa picha mtandaoni inayomuonesha akifanyiwa vituko na staa mwenzake, Kajala Masanja, Mzee Majuto alisema watu wasimfikirie ndivyo sivyo kwani yeye wasanii wengi wa kike wamemgeuza babu yao.
Mzee Majuto akiwa na Odama.

“Wasanii wengi wamenizoea sana, huwa wananitania mara kwa mara na miye nawachukulia kama wanangu hasa hawa mastaa wa kike tofauti na wanaume, sijawahi kuwa na uhusiano na staa yeyote kati yao,” alisema Mzee Majuto.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
27 Dec 2014

Post a Comment

 
Top