Maiti kumi na wawili wanaosadikiwa wame kufa maji katika ajali ya boti iliyotokea wiki moja iliyopita Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo katika Ziwa Tanganyika wameonekana katika ufukwe wa Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma .
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali mstaafu Issa Machibya amesema maiti hizo zimeonekana jana wakielea katika katika kijiji cha Kalilani , tarafa ya Buhingu Wilayani Uvinza.
Amesema kwa kushirikiana na ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo uliopo Kigoma, maiti hao ambao wamekwishaopolewa wa tazikwa leo katika kijiji hicho.
Kwa upande wake , Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt.Lenard Subi am esema kabla ya kuzikwa maiti hao watafanyiwa utambuzi wa kisayansi.
Tarehe 14 mwezi huu Boti inayoitwa MV.Mutambala ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inayofanya safari zake Mashariki mwa nchi hiyo katika Ziwa Tanganyika ilizama na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 120 na wengine 221 wameokolewa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment